Matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na kuuawa kwa msemaji wa kijeshi wa kundi la waasi la M23 Willy Ngoma, serikali ya Kenya ilizindua zoezi la usambazaji wa dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, LENACAPAVIR, UN ulisema taifa la Sudan Kusini, linatoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi elfu 64, watu 25 waliuawa katika jimbo la Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria, pia awamu ya tatu ya mazungumzo ya kidiplomasia kuhusu mradi wa Nyuklia wa Iran, yalifanyika juma hili huko Geneva Uswiz
2026-02-28 07:05:44